Je, mwanamke anajisikiaje akijamiiana na mwanaume aliyevaa kondomu au aliye “peku”?
Hatuwezi kusema mwanamke husikia raha gani akijamiiana na mwanaume
aliyevaa kondomu au na mwanaume asiyevaa kondomu. Kila mtu ana upendeleo
wake, lakini jambo la msingi katika kujamiiana ni hisia, hali ya
kuelewana katika mapenzi na kiwango cha msisimko.
Wanawake wengine wanapendelea kujamiiana na mwanaume aliyevaa kondomu, kwa sababu hofu ya kupata mimba au kuambukizwa magonjwa ya zinaa haipo. Wanawake wengine wanapendelea kujamiiana bila kondomu. Lakini, pamoja na hatari ya kupata mimba, siku hizi kujamiiana bila kondomu kuna hatari ya kuambukizana magonjwa ya zinaa na hasa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kwa hiyo ni vizuri zaidi kutomwamini mtu yeyote mpaka mpimwe kliniki wote wawili kuwa ni wazima wa afya na kuendelea kuwa waaminifu wote wawili.

Post a Comment