Loading...
Home »
Unlabelled »
FAHAMU SABABU ZA KUTOKA HARUFU MBAYA UKENI NA NAMNA YA KUJIKINGA PAMOJA TIBA YAKE MBADALA

Wanawake
na watu wengi huzani kuwa harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya
uchavu na kutojisafisha vizuri… Matokeo yake huongeza jitihada katika
kujisafisha bila mafanikio ya kuondokana na tatizo hili… Kihalisi,
badala kusuluhisha, unapojisafisha zaidi ni unaongeza tatizo badala ya
kutatua…
Japokuwa
ni kweli mara nyingine inaweza ikawa ni sababu ya uchafu… Ila mimi
naamini walio wengi huwa wanazingatia usafi… Ndo maana nimeona leo
tupeane mawazo juu ya tatizo hili, na kujua namna ya kujikinga
VISABABISHI
i. Bacteria
Tatizo
hili husababishwa na Bakteria kwa asilimia kubwa. Kwa asili, ukeni
huishi jamii ya bacteria waitwao Lactobacillus ambao jukumu lao kubwa ni
kufanya mazingila ya uke kuwa katika hali nzuri. Kutokana na njia mbaya
za kusafisha uke,
hasa
kujisafisha kupindukia, ama kwa kutumia sabuni zenye dawa, husababisha
bacteria hawa kufa kwa wingi na mahala pake kuchukuliwa na aina zingine
za bacteria ambao huzaana kwa wingi na kusababisha tatizo hili.
Pia
kwa wale wanaojamiiana kinyume na maumbile, kuna hatari ya kuhamishia
bacteria wanaoishi kwenye njia ya haja kubwa na kuwaamishia ukeni ambapo
watazaliana na kukuletea madhala haya.
ii. Kuvu(fungus)
Hii mara nyingi huambatana na uchafu mzito utokao ukeni mfano wa maziwa mgando(mtindi)
iii. Magonjwa ya zinaa(STIs)
Kwa
asilimia kubwa husababisha na Chlamyidia na kisonono(gonorrhoea). Yote
mawili hutibika kirahisi, ila husababisha madhala makubwa zaidi
yasipotibiwa kwa wakati.
Tukio
baya ni kuwa mwanamke anaweza akawa na magonjwa haya na asione dalili
yoyote. Ila mara nyingine mwanamke anaweza kujisikia maumivu anapokojoa,
na mara nyingine mkojo unakuwa kama una ukungu, vikiambatana na harufu
mbaya.
iv. Maambukizi ya via vya uzazi vilivyo ndani ya nyonga[Pelvic Inflammatory Diseases(PID)]
Hii husababishwa na bacteria waambukizwao kwa njia ya ngono wanapofanikiwa kufika kwenye tumbo la uzazi na hata
pia
mirija ya mimba na hata kokwa(ovaries), hasa chlamydia. Mara nyingi
mwanamke anaweza asijisikie chochote hadi pale atakapojisikia maumivu
yasiyokwisha ya tumbo(chini ya kitovu), au itakapoingiliana na utungaji
wa mimba. Na kama
atajisikia,
mara nyingi huwa ni maumivu ya nyonga, harufu mbaya, uchafu mzito
ukeni, homa, maumivu wakai wa kukojoa na hata maumivu wakati wa
kujamiiana.
Tatizo hili lisipotibiwa mapema laweza kusababisha utasa, ama mimba kutunga nje ya mji wa mimba.
v. Kansa ya uke na kansa ya shingo ya kizazi
Asilimia
chache sana ya wanawake inaweza ikawa ni kutokana na kansa ya shingo ya
kizazi ama ya uke. Hapa ndipo inapoonyesha kuwa tatizo hili siyo la
kufumbia macho, na umuhimu wa kuwahi kwa wataalam wa tiba kwa uchunguzi
wa mapema na kabla tatizo halijawa kubwa.
vi. Uchafu
Usipokuwa
msafi kwa kiwango kikubwa utakuwa unakaribisha wadudu kuzaliana na
kukuletea madhala. Pia unatakiwa kuwa makini wakati wa hedhi, na pia
uchaguzi wa pedi, kwani kuna pedi ambazo zina kemikali za kukata harufu
zinaweza kukudhulu.
JINSI YA KUJIKINGA
•
Usiwe unaosha ukeni kupita kiasi kwani husababisha kuondoa bacteria wa
asili wa ukeni(Lactobacilli) na kukaribisha bacteria wenye madhala.
• Pia epuka sabuni zenye dawa(antibacterial soap) usafishapo ukeni, kwani hii pia huua bacteria wa asili wa ukeni.
• Hii haimaanishi usiwe unasafisha ukeni. Usafi ni muhimu, kwani uchafu pia hukaribisha vimelea vya magonjwa.
•
Kama tatizo limeshajitokeza, wahi haraka kwa wataalam wa tiba
wakufanyie uchunguzi na kujua ni kipi kati ya vilivyotajwa hapo juu
kilichosababisha. Daktari atakuchunguza na kujua kama ni bacteria,
fungus ama ni dalili za awali za kansa na kuchukua hatua mapema kuepusha
madhala zaidi.
• Kumbuka kujisafisha kupindukia si suluhisho kama tatizo limeshajitokea, kwani kunaweza kuzidisha tatizo badala ya kusuluhisha.
DAWA YA KUTOA HARUFU UKEENI
Hii inawatesa wanawake wengi,hadi wanaharibika kisakolojia.anakuwa ana amua kuishi bila ya mwenza.HARUFU ya
ukeni.chemsha hiliki kilo 1
ikipowaa [unachuja na kubakia maji mbali na maganda ya hiliki mbali] nawa sehemu ya Siri [ukeni] asubuhi na
jioni.kwa muda wa wiki2.Hali hiyo ya kutoa harufu
itaondoka. Kama haujapona utaendelea kwa muda siku 30. Kwa uwezo wake Mungu utapona.
Sunday, 14 June 2015
Post a Comment