TATIZO LA UUME KUSINYAA
Mwanaume anayepatwa na tatizo hili anapokuja kujigundua huona kama
mabadiliko makubwa yaliyotokea ghafla katika viungo vyake vya siri.
Mwanamke mwenye tatizo hili pia naye huona kama tatizo geni linaloanza
ghafla.
Kwa kawaida hali hii hutokea katika umri mkubwa kwa mwanaume na mwanamke
yaani kuanzia umri wa miaka hamsini lakini ikitokea katika umri chini
ya miaka hamsini basi ni tatizo. Wapo vijana wenye matatizo haya ambayo
vyanzo vyake tutakuja kuviona katika safu hii.
CHANZO CHA TATIZO
Hali ya kusinyaa kwa viungo vya uzazi kwa mwanamke na mwanaume hutokana
na kuwepo kwa msukumo hafifu wa damu sehemu hiyo, maambukizi sehemu za
siri ambayo huwa ya muda mrefu hasa kaswende, hitilafu katika misuli ya
uke na sehemu za siri za mwanaume inayoathiriwa na kaswende virusi vya
HIV, ugonjwa wa kifua kikuu na hata baadhi ya magonjwa sugu ya ngozi.
Matatizo mengine yanayochangia hali hii ni ugonjwa wa kisukari.
Matatizo katika mishipa ya damu vilevile huweza kusababishwa na magonjwa
ya moyo au mishipa ya damu inayosambaa sehemu hizo. Misuli inaposinyaa
kwa mwanamke nayo huweza kusababishwa na magonjwa kama tulivyoona, uke
unasinyaa pia huweza kusababishwa na uzazi wa mara kwa mara na karibu
kufanya ngono mara kwa mara na wanaume tofauti na hitilafu katika mfumo
wa homoni.
Mwanamke anapata tatizo hili la kusinyaa uke endapo pia homoni au
kichocheo cha Estrogen' kitakuwa kimepungua mwilini na kufanya mafuta
yapungue ukeni. Kwa upande wa mwanaume homoni inayopungua kwa mwanaume
ni Testosterone.
DALILI ZA TATIZO
Mwanaume mwenye tatizo hili hasa kijana, ingawa kwa wazee ni hali ya
kawaida, kijana huanza kuona mfuko wa pumbu hulegea na kushuka sana,
usinyaa na kujikunja kunja, kokwa huinekana ndogo na mishipa mikubwa ya
damu huanza kujitokeza na mishipa mbegu toka katika kende huonekana
wazi. Uume huwa kama wa mtoto mdogo na mishipa ya damu huchomoza wazi.
Nguvu za kiume hupungua sana na endapo ukiweza tendo la ndoa la kwanza
unawahi kumaliza na kushindwa kabisa kupata tendo la pili.
Mara kwa mara maandalizi kabla ya tendo la ndoa kwa mwanaume mwenye
tatizo hili ni kuchezea sana uume kwa kuurusharusha au kuupiga piga
kidogo kidogo ili kuamsha au kuhamasisha msukumo wa damu. Baada ya hapo
uume huanza kusimama taratibu na endapo utasimama basi inabidi uwahi
tendo na kama utachelewa, basi uume utalala na kushindwa tena kufanya
tendo kwa siku hiyo.
Mwanamke yeye daima huwa mkavu na wakati wa tendo hapati hisia zozote
hadi tendo linapokwisha na kama mwanaume hana tatizo lolote na mwenye
nguvu za kutosha basi mwanamke atapata michubuko na maumivu na kuhisi
karaha ya tendo na hawezi kufika kileleni.
UCHUNGUZI
Tatizo hili kama tulivyoona husababishwa na magonjwa mbalimbali, pia
yapo matatizo na magonjwa mengine yanyochangia hali hii, magonjwa kama
kisukari, endapo ugonjwa utakuwa wa muda mrefu unaweza kuathiri hali
hii.
Tabia ya kujichua kwa mwanaume na mwanamke pia huweza kuathiri au
kusababisha tatizo hili kama mtu atakuwa amejichua au kupiga punyeto kwa
muda mrefu kwani msukumo wa damu sehemu za viungo vya uzazi utakuwa
umeathiriwa.
Viungo vya uzazi vinaweza kupooza kutokana na hitilafu katika mishipa ya
fahamu. Mishipa ya fahamu inapoathirika viungo hupooza (paralysis of
genitalia) na mwanaume kushindwa kabisa kufanya tendo la ndoa na ukeni
hakuna kabisa mawasiliano yanayoleta msisimko.
Vipimo vya damu na mkojo na vingine ambavyo daktari ataona vinafaa vitafanyika.
MATIBABU NA USHAURI
Tiba hutolewa kadiri daktari atakavyoona inafaa. Matibabu hutolewa
katika kliniki za matatizo au magonjwa ya kinamama ambapo na kina baba
hutibiwa matatizo haya.
Baada ya uchunguzi tiba itatolea kuona kama hitilafu ni maambukizo au
katika mfumo wa homoni. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba zaidi.



Post a Comment