Loading...
Home »
Unlabelled »
Suluhisho rahisi kwa wanaodhani wamepungukiwa nguvu, wanaosumbuka kurudia tendo au kuwahi kufika
Salaam sana Wakuu
Inavyoonekana siku hizi japo kweli kuna tatizo la upungufu wa nguvu za
kiume haswa kwa mazingira ya mijini, Lakini hili tatizo linaonekana
kukuzwa kuliko lilivyo hadi imepelekea woga mkubwa kwa baadhi ya wengi
wetu.
Ndipo kwenye tafakari yangu nikaona NIANZISHE HUU UZI kwa machache tu
kwa ufahamu mchache nilio nao, Ili NIWAALIKE wengi WENU kwa msaada
zaidi wa mawazo kwa ndugu zetu wanaokutana na mfadhaiko huu.
Nikiamini pia wengi wenu mna utaalamu na mnaoweza kuchambua haya makitu
kwa ufanisi zaidi mkatatusaidia sana kwenye uzi huu. Yafaa sasa
tujikite kwenye ufumbuzi kuliko kuripoti tatizo na kulaumu. Kadiri
tunavyoendekeza kuripoti tatizo tunawaathiri hata wale waliokuwa wazima
ambao kwa kuwa hakuna kipimo sawia kujua kipi ni kipi, nao wasiwasi
unawafanya wanapoteza ujasiri wao na kujiona wana tatizo kumbe wapo
imara sana kuliko mkuki.
Kwa kuanzia yafuatayo yaweza kusaidia kuboresha kulifurahia tendo la ndoa zaidi na kwa muda zaidi.
Kuuweka Mwili vizuri: Ni wazi kuwa tendo hili linachagiwa sana na
mzunguko mzuri wa damu. Mwili ukiwa kwenye hali nzuri kiafya na tendo
huwa linaenda ipasavyo. Na mwili ukiwa dhoofu basi tegemea tukio dhoofu
pia. Hivyo ukitaka kuwa na matokeo mazuri kwenye ndoa yako, jitahidi
sana kujiweka vizuri kwa kula sahihi na kufanya mazoezi mepesi mepesi tu
kwa wale wanaoweza kuutumia muda vizuri wapiti pite Gym walau siku
mbili na kuendelea kwa wiki.
Kufahamu kuwa kupumzika kwa uume baada ya baada kufika mara ya kwanza sio tatizo.
Kwa wanaume walio wengi, baada ya mshindo wa kwanza hupumzika kidogo
kabla ya kuendelea na awamu nyingine. Japo kuna ambao wana uwezo wa
kuendelea moja kwa moja bila kupumzika (law ya use and misuse inahusika
kwa wengine apa). Kwa hio kusinyaa kwa uume baada ya mshindo wa kwanza,
isifahamike kuwa ni upungufu wa nguvu bali ni ajdustiment ya mwili
wenyewe kutokana na kwamba mwanaume kabla ya tendo mapigo ya moyo
huongezeka na huchangia damu kwenda kwa kasi, na kwa hali hio anakua
yupo juu sana kimhemko, inapofikia anamaliza raundi ya kwanza mwili
unakua unapoa /umesharudi
kwenye hali yake ya kawaida, ndiko kunakosababisha hio maneno kusinyaa
kwa wengi wakati mapigo ya moyo yanaporudi kawaida (MWILI KUPOA).
Maandalizi ya mwili. Wanaume tupo tayari muda wote… ila linapokua swala ya mwenza wako (kwa kuwa muda unaotumia kwa maandalizi na tendo una uhusiano wa moja kwa moja na satisfaction ya mwenzio)… unahitaji muda angalao nusu saa na kuzidi kujiandaa na mwenzi wako. Kama timu ya mpira inapoenda ugenini huhitaji muda kuzoea mazingira,
ndio na mwanaume anavyohitaji muda kuzoea mazingira ya ugenini. Hili
linakusaidia sana mwanaume kutoka kwenye mihemko na kurudi kwenye hali
yako ya kawaida ambayo itakusaidia kuwa na muda mzuri zaidi wa kufurahia
tendo. Jitahidi pia kuvuta pumzi nyingi ndani na uiachie polepole
kukusaidia kukuweka kwenye utulivu mzuri.
Timing ya kuanza tendo: Kwa kuwa tendo linahusisha sana hisia
za mwili, ukiwa umetumia muda unaotosha kuandaana, basi usiwe na papara
mwanzoni, bali uwe na utulivu, pia jitahidi kuzungumza moja mawili
wakati unaanza kuzoea mazingira mengine (core business) EPUKA UHARAKA na
kuweka sana akili yako hapo, jinafikie mwenyewe kuwa its just a normal
thing (mental pride)
Concetration/ Umakini uliopitiliza… Unapaswa kumfanya mkeo aweke
akili yake yote hapo, na wewe unatakiwa katika kumuweka mkeo kwenye
concentration uuharibu umakini wako (level of concentration). Ukiweka
concentration ya juu sana kwenye tendo… haikuchukui dakika mbili
umemaliza, na kuirudisha tena ile hali ya concentration uliokua nayo
mwanzo itakuwia ngumu sana….. Usiweke sana akili yako hapo kama unataka
kufurahia kwa muda zaidi. ila kama hutaki kudumu.. weka akili na umahini
wako hapo woote.. just seconds or a minute you are done
MAZOEZI ya mwili ni muhimu sana sana sana sana sana kwetu
wanaume. Kama huna muda wa kwenda jimu walau ukiamka piga ‘PUSH-UPS
walau 50’’ kila siku na ‘’SQUARTS’’ . haya ni mazoezi mepesi lakini ni
BORA zaidi kwa mwanaume. Kwetu sisi wanaume tunatumia sana misuli yetu
wakati huu, kwa hio kuna ulazima wa kutafuta ustahimilivu wa misuli
''mussle strength n perseverance''. Hio kitu ni starehe na unatakiwa
baada ya tendo uwe umekuwa refreshed na sio uwe unaumwa kila mahali na
sijui joints zinauma sijui nini nini? ukijiona unakuwa hivyo baada ya
tendo ujue mwili wako haujakaa fiti ipasavyo kimazoezi/kiafya
Pia Afya
ya Akili inahusika sana, Japo inahitaji jitihada makhususi... lakini
kila mtu ana uwezo wa kuchagua nini cha kufikiria na nini si cha
fikiria(kupuuzia) na pia akienda hatua zaidi anaweza kupuuza kila kitu
kwa wakati fulani kama unajua una huo uwezo na ukaamua kuutumia. Pia
kuchagua kufikiri yale yaliopo kwenye uwezo na urefu wa kamba yako
pekee; vitu usivyo na uwezo navyo utajisumbua tu bure na kujipa stress
zaidi. Weka nguvu na jitihada zako kwenye kutafuta ufumbuzi wa
changamoto zako, jifunze na acha kufikiria matatizo kwa maana
hakubadilishi kitu na yataendelea kuwa hivyo n.k n.k................
Ukiwa na namna nzuri ya kuyachanganua mambo yako utasaidika sana kwenye
afya ya akili yako na kuwa vizuri zaidi
Karibuni wadau kusaidia utatuzi wa hili jinamizi linalojizolea umaarufu kadiri siku zinavyokwenda kwenye jamii yetu.
Friday, 12 June 2015
Post a Comment