
Jana nimesoma makala ya Freddy Macha kwenye gazeti la Mwananchi
iliyokuwa inaongelea mijadala inayoendelea kwenye mitandao mbali mbali
ikieleza kuwa wanaume wa Kitanzania (na labda Waafrika wote) hatujui
mahaba (romance)!
Nimeguswa sana na makala hiyo. Si kwa sababu napingana na hoja za hao wanaosema hivyo, bali nina wasi wasi kwamba vigezo vinavyotumiwa vinaweza kuwa siyo sahihi.
Inawezekana hii mada ilishajadiliwa hapa pia, ila naomba tu kupata maoni ya wadau wa jukwaa letu hili tukukufu kuhusiana na issue hii.
1. Ni kweli wanaume wa Kitanzania hawajui mahaba??
2. Kama hawajui, ni kosa lao peke yao au na wenzi wao (wanawake)???
3. Na vigezo gani vinatumiwa ku-judge kama mtu anajua mahaba au la?
Naomba maoni yenu!!


Post a Comment