
Mtumishi
Fredrick Kishindo ‘Badoo’ akijistili kwa kanga baada ya fumanizi
hilo.Ohoo, ama kweli dunia imekwisha! Mtumishi wa Mungu (Muinjilisti)
ambaye kipindi chake cha dini kinarushwa katika kituo kimoja maarufu cha
televisheni Bongo (Jina tunalihifadhi) aliyefahamika kwa jina la
Fredrick Kishindo ‘Badoo’ hivi karibuni alipata aibu ya mwaka 2015 baada
ya kunaswa na mke wa mtu chumbani, mkanda nzima huu hapa.
Awali
chanzo cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa,
Januari 11, mwaka huu Muinjilisti huyo anayesifika kwa kuhubiri watu
waache dhambi alionekana akinyata kuingia kwenye nyumba ya mke wa mtu
huyo iliyopo Sinza jijini Dar huku kukiwa na taarifa kuwa, mume wa
mwanamke huyo alikuwa safarini.
Wifi mtu atonywa
Ikaelezwa
kuwa, kufuatia mazingira hayo wifi wa mwanamke huyo alitonywa juu ya
taarifa za Badoo kuingia kwenye nyumba ya kaka yake, maelezo
yaliyomshitua hivyo kulazimika kuelekea eneo la tukio.
Baada
ya wifi mtu huyo kufika nyumbani kwa kaka yake na kuhakikishiwa kuwa
Badoo yuko ndani, aliuliza namna ya kuwapata makamanda wa Operesheni
Fichua Maovu ya Global Publishers ‘OFM’ ambapo mmoja wa majirani
alimpatia namba ya simu, akawapigia.
...Akivaa shati huku kitendea kazi chake(Biblia) kikiwa nyuma yake. Polisi washirikishwa


Post a Comment