Saikolojia na maisha
Malalamiko yanayotolewa na
baadhi yao yanaonesha kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu
dakika na dakika tatu kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu
katika hatua za awali tu za hamasa ya kimahaba.
Hata hivyo,
kumetolewa maelezo na nafuu ya ongezeko la muda katika tendo la pili na
kuendelea, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya
wanawake limekuwa likiwahuzunisha wanaume wengi.
Ni ukweli
usiopingika kuwa, mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya mwenzake
humsababishia kero mwanamke anayeshiriki naye tendo, kwani humwacha njia
panda pasipokuwa na hitimisho la raha ya kujamiiana.
Hali hii
inatokana na maumbile ya uume wa mwanaume ambao husinyaa mara baada ya
kuhitimisha mbio zake, lakini kwa mwanamke kuwahi si tatizo, kwani
hakumfanyi ashindwe kumsindikiza mwenzake hadi kileleni.
Utofauti
huu ndiyo unaowafanya wanaume wahuzunike zaidi wanapokabiliwa na janga
hilo kiasi cha kufikia hatua ya kwenda kwa waganga/matabibu ili
iwasaidie kuepuka balaa ya kutoka uwanjani na aibu.
Ingawa
kumekuwa na mafanikio katika tiba za kisayansi, lakini bado wanaume
wameshindwa kupata ukombozi wa kudumu wa tatizo hili. Wengi wamejikuta
wakijiongezea mzigo wa fikra kwa kuzitumaini zaidi dawa au kuzitumia na
kupata matokeo mabaya zaidi ya kuishiwa nguvu kabisa.
Kwa
kufahamu mikinzamo iliyopo kati ya akili na tiba ya nguvu za kiume na
madhara yachipukiayo imebainika kuwa, mtu anaweza kujitibu tatizo hilo
kwa kutumia kanuni za kisaikolojia na mafanikio yasiyo na madhara
yakapatikana.
Wataalamu wa kisaikolojia wanatambua kuwa kanuni ya ufanyaji mapenzi iko zaidi kwenye ubongo kuliko mwilini.
Kinachotokea
hadi mtu akapata msisimko wa kufanya mapenzi si mwitikio wa mwili, bali
ni utambuzi wa akili juu ya kiwango cha mapenzi kilichopokelewa kwenye
ubongo unaojihusisha na hisia.



Post a Comment