Saratani
ya matiti ni ugonjwa ambao huwapata wanawake na unatokana na athari za
chembe ndogo ama seli kwenye matiti na matokeo yake ni kwamba hubadili
mfumo wa kawaida wa kukua na kuongezeka.
Mabadiliko
haya huanza polepole na yanaweza yakachukua muda mrefu hadi mtu kuweza
kujua kama ana matatizo hayo. Ikiwa katika hatua hizo za mwanzo kwa
kawaida huwa haina maumivu jambo hilo ni moja ya mambo ambayo huchangia
baadhi ya wagonjwa kubaini tatizo hilo wakati tayari limekomaa.
Ni
kutokana na sababu hizo, wanawake hutakiwa kuchunguza afya zao mara kwa
mara kwa sababu ugonjwa huweza kutibiwa kirahisi iwapo utabainika
mapema, miongoni kwa dalili mwa dalili za saratani ya mititi ni uvimbe
kwenye matiti ama makwapa. Titi kubadilika kiumbo, titi kutoa majimaji
yakiyochanganyika na damu ama chuchu kuingia ndani.
Dalili
zingine ni rangi ya ngozi ya titi kubadilika na kuonekana kama ngozi ya
nje ya chungwa na ile hali yake ya kuonekana kuwa na ngozi laini
hutoweka.

Mwanamke
anaweza kujinguza mwenyewe maradhi haya ya saratani na kujua kama
ameathirika ama la, kabla ya kufanya uchunguzi huu unapaswa kufahamu
masharti yafuatayo:
Kama
anayejichunguza ana umri zaidi ya miaka 20, anapaswa kuhakikisha
anaufanya katika siku ya tano, sita na saba baada ya kumaliza hedhi.
Unapaswa kufuata hatua kwa hatua katika uchunguzi huo. Hizi ni hatua
zifuatavyo:
Utakiwa
kuwa na kioo kikubwa kiasi ambachoo waweza kujiona vyema angalau kifua
chote. Tafuta sehemu ambayo mwanga utakuwa unakupiga kifuani na kioo
kuwa mbele yake.

Hii
mara nyingi inapaswa kufanywa chumbani ambako mtu aweza kupata faragha
kwa kuwa itampasa kuvua nguo angalu kifua kukiacha wazi. Kioo hicho
waweza ukawa umekitundika ukutani ama sehemu yoyote ambayo utajiona vema
ukiwa umesimama.
Vua
nguo na kuhakikisha kifua na tumbo lipo wazi. Hatua ya kwanza jiangalie
kwenye kioo ukiwa umesimama wima na umeweka mikono kiunoni. Angalia
kama kuna mabadiliko katika umbo au rangi ya ngozi ya matiti na kama
chuchu zinaonekana kutumbukia ndani ya titi.
Unaweza
kulinganisha rangi kwa matiti yote mawili na kuona kama zinafanana.
Kama yanatofautiana yawezekana kuna athari, pia kama moja ya titi
litaonekana chuchu imeingia ndani, pia ni moja ya viashiria vya athari
ya aina hii ya saratani.
Hatua
ya pili, nyanyua mkono juu na viganja vishikane juu ya kichwa chako.
Hapa chunguza kama kuna mabadiliko yoyote katika mlingano wa ukubwa wa
matiti. Kama moja litaonekana kuwa kubwa zaidi ya jingine pia ni moja ya
viashiria vya athari.

Hatua
ya tatu, hii haihitaji kioo, unachotakiwa kufanya ni kusimama wima na
kunyanyua mkono wa kushoto juu huku vidole vya mkoo wako wa kulia vikiwa
vinabinya na kuachia kwa mzunguko kwenye titi kuangalia kama ndani kuna
uvimbe.
Baada ya kumaliza kwa titi la kushoto vivyo hivyo utafanya kwa titi la kulia. Njia hii pia waweza kuifanya ukiwa umelala chali.
Hatua
ya nne, ni ya kuchunguza matiti kwa kukamua na kuangalia kama kuna ute
uliochanganyika na damu. Iwapo utakuwepo wa namna hiyo basin i kiashirio
kwamba kuna uwezekano wa kuwa na athari za ugonjwa huu.
Yawezekana
ukawa na uvimbe ama kitu kingine chochote lakini ikawa ni matatizo
mengine yasiyohusu saratani. Wataalamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti
ndio watakaothibitisha kama una atahri hizo na si vinginevyo.
Wataalam waliofanya utafiti juu ya saratani ya matiti walibaini kwamba hali hiyo inaweza kusababishwa na sababu mbalimbali.
Sababu
hizo ni kama vile kuanza hedhi katika umri mdogo, kukoma hedhi katika
umri mkubwa, mwanamke kufikisha umri bila kuzaa na utumiaji wa mafuta
mengi katika mlo.
Mambo
mengine yanaweza kuchangia saratani ya matiti ni mama kutonyonyesha
baada ya kujifungua ana kumnyonyesha kwa muda mfupi. Kuna kina mama
wenye tabia ya kutaka, kutonyonyesha kutokana na sababu zao mbalimbali
ambazo mara nyingi siyo za msingi.
Mambo
mengine ambayo yanachangia mtu kupata saratani ya titi ni unene kupata
kiasi, kutofanya mazoezi mara kwa mara, uvutaji wa sigara, matumizi ya
pombe kupita kiasi, wa wakati mwingine inaweza kurithiwa kutokana na
historia ya saratani ya matiti katika jamii husika.
Mgonjwa
wa saratani ya matiti aweza kupata tiba na kupona kabisa hivyo hakuna
haja ya kuwa na wasi wasi. Hata hivyo, kama nilivyoeleza awali, mtu
anapaswa kuibaini mapema kwa sababu ni wakati ambao anaweza akapatiwa
tiba na kupona kwa urahisi.
Aina
zote za saratani ni kwamba zinapaswa kuibainiwa mapema kwa kuwa hiyo
ndiyo njia pekee ya kuweza kuitibu na kupona bila ya mtu kupata matatizo
mengi. Zipo aina mbalimbali za tiba na mojawapo ni upasuaji. Upasuaji
huu kwa kawaida hufanywa katika hatua za mwanzo.
Njia
nyingine ni tiba ya mionzi au kupewa dawa. Jambo la kukumbukwa ni
kwamba ugonjwa huu unaweza kusababisha kifo iwapo hautabainika mapema na
kupatiwa tiba mwafaka.
Njia
ambayo mtu aweza kujilinda asiathirike na saratani hii ya matiti ni
kujichunguza mara kwa mara ili kubaini mapema ma kupatiwa dawa.
Kwa kawaida ,mwanamke anapaswa kuchunguzwa mara moja kwa mwaka ili kuona kama ameathirika na ugonjwa huo au la.


Post a Comment